IQNA

Mzoga watupwa msikitini Canada, mshukiwa akamatwa kisha aachiliwa

20:46 - December 14, 2021
Habari ID: 3474674
TEHRAN (IQNA)- Polisi nchini Canada imemkamata mtu mmoja Jumatatu baada ya mzoga kutupwa nje ya msikiti katika eneo la Vaudreuil-Dorion hivi karibuni.

Msemaji wa polisi anasema wamemkamata mshukiwa mmoja mwenye umri wa miaka 33 Jumatatu.

Mtu huyo ameachiliwa baada ya kukubali kufuata masharti kadhaa ikiwa ni pamoja na kuripoti kortini endapo atafunguliwa mashtaka.

Msemaji wa polisi amesema yamkini mtu huyu akakabiliwa na kosa la jinai la kusababusha usumbufu na kueneza chuki.

Mzoga wa mnyama ambaye hakutajwa ulipatikana nje ya Kituo cha Kiislamu cha   de Vaudreuil-Soulanges  eneo la Rang St-Antoine jimboni Quebec nchini Canada. Jengo hila la msikiti liliwahi kuwa mgahawa na baa kabla ya kununuliwa na Waislamu na matumizi yake kubadilika. Hatua hiyo imepingwa na baadhi ya wakazi wa eneo hilo.

Uislamu ni dini inayoenea kwa kasi zaidi Canada ambapo Waislamu wameongezeka kwa asilimia 82 katika kipindi cha muoongo moja uliopita. Hivi sasa Waislamu ni karibu asilimia 3.5 ya watu wote milioni 38 nchini Canada.

Disemba mwaka 2017, Trudeau katika ujumbe wake kwa Kongamano la Kuhuisha Uislamu alisema Waislamu nchini Canada wamekuwa na mchango mkubwa na ni rasilimali muhimu kwa nchi.

"Canada ina bahati kuwa na jamii ya Waislamu wenye harakati," alisema Trudeau katika ujumbe wake maalumu kwa njia ya video.

"Kwa muda wa miaka mingi, Waislamu nchini Canada wameweza kupata ustawi na kutoa mchango mkubwa kwa jamii  huku wakiwa wanadumisha ufungamano muhimu na nchi zao za asili na jambo hilo limewawezesha kuwa na turathi nzuri ya utamaduni."

Pamoja na hayo nchini hiyo imekuwa ikishuhudia vitendo vya chuki dhidi ya Waislamu mara kwa mara.

3476929

captcha