IQNA

Iran yasema Sweden iwajibike kuhusu kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu

17:22 - April 17, 2022
Habari ID: 3475132
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema serikali ya Sweden inapaswa kuwajibika kuhusu kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini humo.

Katika taarifa, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Sweden Saeed Khatibzadeh ametoa kauli hiyo baada ya mhalifu mmoja mwenye misimamo ya kufurutu ada wa mrengo wa kulia nchini Sweden amechoma nakala inayoaminiwa ni ya Qurani Tukufu katika mtaa ambao akthari ya wakazi wake ni Waislamu.

"Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalaani vikali kitendo cha kuchoma moto nakala ya Qur'ani Tukufu katika mji wa Linkoping nchini Sweden. Kitendo hicho kimetekelezwa na raia wa Denmark mwenye misimamo mikali kwa kisingizio cha 'uhuru wa maoni' na kwa uungaji mkono wa polisi ya Sweden," amesema Khatibzadeh.

Aidha msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kukaririwa kwa makusudi kitendo hicho kiovu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni jambo ambalo limeumiza hisia za Waislamu Sweden na duniani kote.

Khatibzadeh amesema kitendo hicho kilichojaa chuki ni ukiukaji wa uhuru wa maoni na kinapaswa kulaaniwa na wote wanaoamini msingi wa mazungumzo na maelewano baina ya dini.

Aidha amesema serikali ya Sweden inapaswa kuwajibuka na kuchukua hatua kali na za wazi dhidi ya waliovunjia heshima Qur'ani Tukufu nchini humo.  Halikadhalika Khatibzadeh amesema kitendo kama hicho kinaonyesha udharura wa kuwepo umoja wa Waislamu na nchi za Kiislamu ili kukabiliana na njama za maadui wa Uislamu.

Katika miezi ya karibuni Sweden imeshuhudia matukio kadhaa ya hujuma na mashambulio dhidi ya Waislamu, maeneo yao matakatifu na kuvunjiwa heshima pia kitabu kitukufu cha Qur'ani.

3478519

captcha