IQNA

Waislamu Sweden washerehekea Maulidi ya Mtume Muhammad SAW

16:58 - November 02, 2020
Habari ID: 3473322
TEHRAN (IQNA) – Waislamu katika mji mkuu wa Sweden, Stockholm wameshiriki katika maadhimisho ya kukumbuka siku ya kuzaliwa (Maulid) Mtume Muhammad SAW na pia uzawa wa mjukuu wake, Imam Jaafar Swadiq AS.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, sherehe hizo zimefanyika katika Kituo cha Kiislamu cha Imam Ali AS mjini Stockholm ambapo, lengo la sherehe hiyo limetajwa kuwa ni kuwaelimisha washiriki kuhusu Utume, Uimamu na shakhsia na Sira ya Mtume Muhammad SAW pamoja na maadili ya Kiislamu na ukarimu wa mtukufu huyo.

Washiriki katika sherehe hizo wamezingatia kanuni zote za afya za kuzuia maambukizi ya corona.

Waislamu wa madhehebu ya Sunni wanaamini kuwa Mtume Muhammad SAW alizaliwa 12 Rabiul Awwal nao Waislamu wa madhehebu ya Shia wanaamini kuwa ni 17 Rabiul Awwal.

Kwa msingi huo, Imam Khomeini MA, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alitangaza kipindi cha kuanzia tarehe 12 hadi 17 Rabiul Awwal kila mwaka kuwa ni Wiki ya Umoja kati ya Waislamu kote duniani. Wiki ya Umoja ni fursa nzuri ya kuzikurubisha nyoyo za Waislamu na kuimarisha umoja na mshikamano wao katika kukabiliana na maadui wa ulimwengu wa Kiislamu.

3932485

captcha