IQNA

Kiongozi Muadhamu kuwahutubia Waislamu duniani kwa mnasaba wa sherehe za Maulidi ya Mtume SAW

15:45 - November 01, 2020
Habari ID: 3473318
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei atahutubu kwa njia ya televisheni kwa mnasaba wa maadhimisho ya kukumbuka siku ya kuzaliwa (Maulid) Mtume Muhammad SAW na pia uzawa wa mjukuu wake, Imam Jaafar Swadiq AS.

Kwa mujibu wa taarifa, hotuba hiyo ya Jumanne tarehe tatu Novemba itaanza saa nne na nusu asubuhi kwa wakati wa Tehran au saa nne asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki na itarushwa hewani na radio na televisheni za Jamhuri ya Kislamu ya Iran ikiwemo Press TV kwa lugha ya Kiingereza, Al Alam kwa lugha ya Kiarabu na Hispan TV kwa lugha ya Kihispani.

Waislamu wa madhehebu ya Sunni wanaamini kuwa Mtume Muhammad SAW alizaliwa 12 Rabiul Awwal nao Waislamu wa madhehebu ya Shia wanaamini kuwa ni 17 Rabiul Awwal.

Kwa msingi huo, Imam Khomeini MA, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alitangaza kipindi cha kuanzia tarehe 12 hadi 17 Rabiul Awwal kila mwaka kuwa ni Wiki ya Umoja kati ya Waislamu kote duniani. Wiki ya Umoja ni fursa nzuri ya kuzikurubisha nyoyo za Waislamu na kuimarisha umoja na mshikamano wao katika kukabiliana na maadui wa Waislamu kote duniani.

3932546

captcha