IQNA

Mashindano ya Qurani

Qari wa Iran ashinda Mashindano ya Qur'ani ya Katara nchini Qatar

22:33 - February 27, 2023
Habari ID: 3476633
TEHRAN (IQNA) – Qari wa Kiirani ameshika nafasi ya kwanza katika toleo la sita la Tuzo ya Katara ya Kuhifadhi Qur’ani nchini Qatar.

Mohammad Hassan Hassanzadeh, kutoka mkoa wa kati wa Iran wa Yazd, aliwasili nchini Jumamosi usiku baada ya kushinda shindano hilo.

Usajili wa shindano hilo ulianza mnamo Septemba 1, 2022, na kuhitimishwa mnamo Novemba 30.

Duru ya awali ilifanyika kwa njia ya intaneti, na washindani kutoka nchi 67 walituma faili za qiraa  kwa kamati ya maandalizi kupitia mtandao.

Wasomaji  Qur’ani mia moja kutoka nchi 13 za Kiarabu na 18 zisizo za walifuzu kuingia finali.

Kulingana na Hassanzdeh, ilijumuisha duru tatu za ana kwa ana zilizofanyika katika mji mkuu wa Qatar wa Doha.

Aliiambia IQNA kwamba washindani waligawanywa kwanza katika makundi matano washindani bora katika kila kundi walifika raundi iliyofuata.

Hassanzadeh aliongeza kuwa hatimaye washiriki watano wakuu, akiwemo yeye, walifuzu kuingia fainali hizo. Makari wengine wanne walikuwa Osama Karbalaei na Ahmed Jamal kutoka Iraq, Sheikh Abdul Razaq Shahawi kutoka Misri na mshindani mmoja kutoka Morocco.

Qari wa Iran alitwaa tuzo ya juu zaidi katika mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani. Mshindi wa pili alikuwa Osama Karbalaei na Sheikh wa Misri Abdul Razaq Shahawi aliibuka wa tatu.

Washindi wa nafasi za tatu za  kwanza walipokea riyal za Qatar  500,000, 300,000 na 100,000 mtawalia.

Kauli mbiu ya toleo la mwaka huu ilikuwa "Ipambeni Qur’an kwa Sauti Zenu”.

Kwa mujibu wa waandaaji, Tuzo ya Katara ya Kuhifadhi Qur'ani inalenga kustawisha vipaji katika kusoma Qur'ani Tukufu; kugundua, kusaidia na kuwatambulisha watu wenye vipaji duniani na halikadhalika kuwaenzi wasomaji mashuhuri na wabunifu; kuwahamasisha vizazi vijana kushikamana na dini yao, na kuwawezesha kutambua wajibu wao kwa imani yao ya Kiislamu.

Iranian Qari Wins Katara Quran Competition in Qatar

Iranian Qari Wins Katara Quran Competition in Qatar

Iranian Qari Wins Katara Quran Competition in Qatar

  4124534

captcha