IQNA

Harakati za Qur'ani Tukufu

Mashindano ya Kimataifa ya Miujiza ya Qur'an ya Misri: makataa ya kushiriki yameongezwa

16:05 - March 02, 2023
Habari ID: 3476646
TEHRAN (IQNA) – Muda wa mwisho wa kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya 'Miujiza ya Qur'ani na Sunnah' umeongezwa kwa miezi miwili, kwa mujibu wa waandaaji.

Kamati ya Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Muujiza wa Kisayansi wa Qur'ani na Sunnah itaandaa mashindano ya kimataifa ya "muujiza wa kisayansi wa Qur'ani na Sunnah katika kuunda uwezo wa binadamu kwa ajili ya kufikia maendeleo endelevu".

Wale walio tayari kushiriki katika shindano hilo wanaweza kuwasilisha makala zao kuhusu mada ya tukio hilo kufikia Aprili 30.

Kamati hiyo ilisema kuongezwa kwa muda huo kumekuja kutokana na ombi la watafiti nchini Misri na nchi nyingine zinazotaka kushiriki mashindano hayo.

Makala hizo zinapaswa kuwa za Kiarabu au Kiingereza, hazijawasilishwa kwa hafla zingine, na hazijachapishwa hapo awali, kulingana na kamati.

Iliongeza kuwa kazi hizo zinapaswa kuwa kati ya kurasa 100 na 150 kwa urefu na kujumuisha muhtasari wa kurasa 10 hadi 20. Washiriki hawapaswi kuwa miongoni mwa wale ambao wameshinda nafasi juu katika mashindano yaliyopita. Washiriki 15 bora watatunukiwa jumla ya pauni 71,000 za Misri.

Pia, makala bora zinazoshiriki katika shindano zitachapishwa kwa kiasi.

4125306

captcha