IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Qarii Mustafa Ismail wa Misri akisoma Aya ya Qur'ani kuhusu Mwezi wa Ramadhani (+Video)

11:56 - March 26, 2023
Habari ID: 3476763
TEHRAN (IQNA) – Ramadhani ni mwezi uliobarikiwa ambapo Mtume Muhammad SAW aliteremshiwa Qur’ani Tukufu. Ni mwezi ambao Waislamu hutumia muda mwingi kusoma na kutafakari kuhusu Qur’ani Tukufu. Ifuatayo ni kisomo cha qarii mashuhuri wa wa Misri marehemu Sheikh Mustafa Ismail kuhusu mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Anasoma aya ya 185 ya Surah Al-Baqarah:

Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru.

 

Sheikh Mustafa Ismail aliyezaliwa Juni 17,1905 katika eneo la Tanta jimboni Gharibia nchini Misri na alikuwa miongoni mwa wasomaji mashuhuri zaidi wa Qur'ani Tukufu nchini Misri.

Alikuwa na mtindo maalumu wa qiraa na aliweza kuwavutia wengi kutokana na usomaji wake. Qarii mashuhuri wa Misri katika zama hizi Sheikh Ahmed Ahmed Noaina amesema, "Mustafa Ismail alikuwa na mbinu kadhaa za qiraa na hadi sasa hakuna mtu aliyweza kuja na mbinu mpya baada yake.

Alianza kujifunza Qur'ani Tukufu na misingi ya Tajwidi kutoka kwa Sheikh Idris Fakhir. Alizana qiraa ya Qur'ani mbele ya hadhara kubwa akiwa na umri wa miaka 4 katika Msikiti wa Atif eneo la Tanta ambapo sauti yake iliwavutia wengi. Aliendeleza kipaji chake kwa kuelekea Cairo ambapo alikuwa mwanafunzi wa Qarii Sheikh Muhammad Rafa'at. Alipata umashuhuri na akaanza kualikwa katika nchi mbali mbali kusoma Qur'ani Tukufu kama vile Iraq, Indonesia, Saudi Arabia, Pakistan, Ujerumani, Palestina, Uingereza na Ufaransa.  Aidha alitunukiwa tunzo kadhaa kitaifa na kimataifa kutokana na umahiri wa qiraa yake ya Qur'ani Tukufu. Hatimaye Sheikh Mustafa Ismail aliaga dunia na kurejea kwa Mola wake mnamo Disemba 26, 1978.

4129108

captcha