IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Katibu Mkuu UN asikitishwa na ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu

10:28 - November 09, 2023
Habari ID: 3477865
NEW YORK (IQNA)- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesikitishwa na kuongezeka vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na pia kile alichokitaja kuwa ni 'chuki dhidi ya Uyahudi'.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X: Picha za uchungu zilisambazwa kutoka Magharibi mwa Asia zinautia simanzi moyo wa mtu.

Guterres aliongeza: "Maneno ya chuki na vitendo vya uchochezi lazima vikome." Nimesikitishwa sana na ongezeko la chuki dhidi ya Waislamu. Lazima tutafute njia ya kuhifadhi ubinadamu wetu tunaoshirikiana.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anasema hayo kati hali ambayo, vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na na Waislamu vimeongezeka mno hususan katika mataifa ya Ulaya.

Katika miezi ya hivi karibuni, nchi za Sweden na Denmark, zikitumia kisingizio cha madai yao ya "uhuru wa kujieleza", zimetoa vibali vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu kwa watu wenye misimamo mikali, na kwa hakika, vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na kuvunjiwa heshima Qur’ani Tukufu vimekuwa vikiendelea kufanyika katika mataifa hayo mawili kwa baraka kamili na uungaji mkono wa serikali za mataifa hayo yaliyoko katika bara la Ulaya.

Vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu vinaendelea kushuhudiwa katika mataifa ya Magharibi katika hali ambayo, nchi hizo daima zimekuwa zikitoa madai ya uhuru wa kujieleza.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anadai kuwa kuna chuki dhidi ya Mayahudi katika hali ambayo kundi hilo ndilo lenye ushawishi mkubwa zaidi katika tawala za Magharibi na hasa Marekani. Kutokana na ushawishi wa Mayahudi,  serikali ya Marekani imalazimika kuupa himaya utawala wa Kizayuni wa Israel ambao hivi  sasa unatekeleza jinai dhidi ya Wapalestina. Wakati wananchi wa nchi za Magharibi wanapoandamana kupinga jinai za Israel huko Gaza na Palestina kwa jumla wanadaiwa kuwa eti wana chuki dhidi ya Uyahudi katika  hali ambayo kile wanachopinga ni jinai za utawala huo wa Kizayuni.

Madola ya Magharibi yanalaumiwa kwa kupuuza kwa makusudi tofauti iliyopo baina ya uhuru wa kujieleza na kutusi au kuvunjia heshima matukufu ya dini.

4180697

captcha