IQNA

Chama cha Kansela wa Ujerumani chataka Kufanya Ujasusi Misikitini

14:18 - May 02, 2016
Habari ID: 3470284
Mwanachama mwandamizi wa chama cha Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema serikali inataka kurekodi na kufanya ujasusi kuhusu hotuba katika misikiti nchini humo.

Mbunge wa chama cha Christian Democratic Union CDU Volker Kauder amesema anataka serikali ifanye upelelezi kuhusu yanayohubiriwa na maimamu misikitini.

"Tunahitaji kuzunguma kuhusu ukweli kuwa baadhi ya hotuba katika misikiti ni kinyume cha ufahamu wetu kuhusu nafasi ya serikali," amesema katika mahojiano na gazeti la Berliner Zeitung.

Katika mahojiano hayo, Kauder amehoji kuhusu sera za serikali ya CDU katika kukabiliana na misimamo mikali miongoni mwa Waislamu. Amesema nchini Ujerumani dini haipaswi kuchukua nafasi kubwa kulika serikali.

Baraza la Waislamu la nchini Ujerumaini kutahadharisha kuhusu kuongezeka vitendo vinavyotokana na chuki za kidini dhidi ya Waislamu nchini humo. Baraza hilo limetangaza kuwa, chuki dhidi ya Waislamu na dhidi ya wageni zimeongezeka nchini Ujerumani baada ya watu wasiojulikana kuwapora na kuwadhalilisha wanawake katika mji wa Cologne katika mkesha wa mwaka mpya wa 2016. Itakumbukwa kuwa, Oktoba mwaka jana kundi la PEGIDA lilitoa wito kuwa Waislamu barani Ulaya wapelekwe kwenye kambi za mateso makali kama zile zilizokuwepo wakati wa utawala wa Kinazi nchini Ujerumani.

3459692

Kishikizo: iqna merkel waislamu
captcha