IQNA

OIC, yalaani kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu Sweden

22:55 - August 31, 2020
Habari ID: 3473123
TEHRAN (IQNA) - Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) sambamba na kulaani hatua ya kuvunjiwa heshima na kuchomwa moto nakala ya Qurani Tukufu nchini Sweden na kusema kitendo hicho kilichofanywa na wafuasi wenye misimamo iliyochupa mipaka wa mirengo ya kulia katika nchi hizo za Ulaya ni cha kichokozi na kichochezi.

Katika taarifa, Katibu Mkuu wa OIC amesema kitendo hicho kinakusudia kuchochea hisia kali na kuumiza nyoyo za Waislamu kote duniani. Amesema vitendo vya namna hii vya kuvunjia heshima matukufu ya kidini havitakuwa na matokea mengine ghairi ya kuvuruga jitihada za kimataifa za kukabiliana na chuki na misimamo mikali ya kufurutu ada.

Nayo Idara ya OIC ya Kufuatilia Chuki Dhidi ya Uislamu imelaani kitendo hicho cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini Sweden na kupongeza hatua zilizochukuliwa na wakuu wa nchi hiyo kukabiliana na jinai hiyo.Taarifa hiyo pia imetoa wito kwa Waislamu wa Sweden wawe watulivi katika kipindi hiki kigumu.

Siku ya Ijumaa, watu wenye chuki dhidi ya Uislamu waliteteteza nakala ya Qur'ani katika mji wa Malmo nchini Sweden. Walioivunjia heshima Qur'ani Tukufu nchini Sweden ni wafuasi wa mwanasiasa mwenye misimamo mikali ya kibaguzi wa Denmark  Rasmus Paludan.

3472414

captcha