IQNA

Mtazamo wa Darul Iftaa ya Misri kuhusu kuandika aya za Qur'ani kwenye noti na sarafu

10:52 - November 02, 2021
Habari ID: 3474503
TEHRAN (IQNA)-Taasisi ya Darul Iftaa ya Misri imesema kuchapisha aya za Qur'ani Tukufu kwenye noti na sarafu ni Makruh.

Katika Uislamu kitu ambacho ni Makruh huwani kitu kisichopendeza au kinachukiza lakini si haramu na wala kukifanya hakuna adhabu. Hatahivyo, iwapo mtu atajizuia nacho basi atapata thawabu.

Darul Iftaa imeandika katika tovuti yake kuwa, wasomi na mafuqaha wa Kiislamu wanasema haifai kugusu Qur'ani Tukufu bila wudhuu.  

Ni kwa msingi huo ndio mafuqaha katika  Darul Iftaa wakasema ni Makruh kuchapisha aya za Qur'ani katika noti na sarafu kwa sababu yamkini zikaguswa na wale ambao hawana Wudhu au wasio watoharifu.

Darul Iftaa al Misriyyah, ni moja ya taasisi muhimu zaidi za kutoa miongozo na Fatuwa za Kiislamu duniani na ilianzishwa mwaka 1313 Hijriya Qamariya sawa na 1895 Miladia.

Taasisi hiyo mara kwa mara hutoa miongozi kwa Waislamu kuhusu masuala ya kila siku katika zama hizo kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.

4009730

captcha