IQNA

Maimamu wa Indonesia kuhudumu katika misikiti UAE

11:52 - November 02, 2021
Habari ID: 3474505
TEHRAN (IQNA) Maimamu 15 kutoka Indonesia wamewasili Umoja wa Falme za Kiarabu kwa ajili ya kuswalisha na kutoa hotuba katika misikiti kote katika nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa maimamu hao ni kati ya 38 ambao wameteuliwa na Idara ya Masuala ya Kiislamu na Wakfu UAE kuhudumu katika misikiti nchini humo.

Maimamu hao watasimamia misikiti katika miji ya Abu Dhabi, Al Ain, Al Dhafra, Fujairah and Ras Al Khaimah kati ya maeneo mengine.

Wahubiri hao wa Kiislamu wamewasili UAE katika fremu ya mradi wa 'Maiamu Kutoka Indonesia' ambao unatekelezwa kufuatia mapatano baina ya Mrithi wa Ufalme wa Abu Dhabi Sheikh Mohamed bin Zayed na Rais wa Indonesia Joko Widodo alipotembelea Abu Dhabi mwezi Januari mwaka jana.

Kwa mujibu wa mapatano hayo, Indonesia itatuma wahubiri wa Kiislamu wapatao 200 kufanya kazi nchini UAE hadi kufikia mwisho wa mwaka ujao.

Balozi wa Indonesia nchini UAE Husin Bagis anasema mradi huo ni dalili kuwa uhusiano baina ya nchi hizi mbili hauko tu katika masuala ya kiuchumi.

Amesema wakati wakiwa nchini UAE maiamu hao watajifunza namna watu wanavyoishi kwa amani na kwa kustahamiliana katika jamii pasina kuwepo mizozo na hivyo wakirejea Indonesia wataeneza sera hiyo hiyo.

Inatazamiwa kuwa mradi huo utapelekea kuwepo mabadilishano ya kielimu baina ya nchi mbili sambamba na kusisitiza kuhusu Uislamu wa misimamo ya wastani.

3476300/

Kishikizo: indonesia uae ABU DHABI
captcha