IQNA

Kadhia ya Palestina

Bunge la Ulaya latoa wito wa kutambuliwa rasmi nchi ya Palestina

21:16 - July 14, 2023
Habari ID: 3477280
BRUSSELS (IQNA)- Katika kikao chake cha hivi karibuni kabisa, Bunge la Ulaya limeutaka Umoja wa Ulaya na nchi wanachama wa umoja huo kuitambua rasmi nchi ya Palestina.

Kwa mujibu wa taarifa, Bunge la Ulaya limesititizia uungaji mkono wake madhubuti kwa "masuluhisho ya serikali mbili" kati ya Wapalestina na Wazayuni katika mipaka ya mwaka 1967.

Katika mkutano wake wa hivi karibuni kabisa uliofanyika mjini Strasbourg nchini Ufaransa, Bunge la Ulaya limeutaka Umoja wa Ulaya na nchi wanachama wake kulitambua rasmi taifa la Palestina.

Bunge hilo pia limetaka kuheshimiwa sheria za kimataifa na kwa mara nyingine tena limetilia mkazo "dhamira ya Umoja wa Ulaya ya kupatikana haki sawa huko Palestina."

Bunge la Ulaya pia limetaka kufanyike uchaguzi wa Mabunge ya Kutunga Sheria na wa Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina haraka iwezekanavyo na kuutaka utawala wa Kizayuni uruhusu uchaguzi huo ufanyike katika eneo la mashariki mwa mji wa Baytul Muqaddas.

Katika kikao hicho imesisitizwa pia kwa mara nyingine tena kwamba vitongoji vya walowezi wa Kizayuni vinavyojengwa kwenye ardhi wanazoporwa Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ni haramu kwa mujibu wa sheria zote za kimataifa na vinapaswa kuvunjwa mara moja na ardhi hizo kurejeshewa Wapalestina wenyewe.

4154984

captcha