IQNA

Siasa

Ni marufuku kutumia neno ‘Israeli’ katika vyombo vya habari vya Iraq

17:21 - January 18, 2024
Habari ID: 3478213
IQNA - Kutumia neno "Israel" katika kuashiria utawala wa Tel Aviv kumepigwa marufuku katika vyombo vya habari vya Iraq, afisa mmoja alisema.

Ali Almuayid, Mkuu wa Kamisheni ya Vyombo vya Habari na Mawasiliano (CMC) nchini Iraq, alisema vyombo vyote vya habari lazima vitumie istilahi ya "utawala wa Kizayuni" badala ya Israel.

Marufuku hiyo imeanzishwa kutokana na matukio ya hivi karibuni katika Ukanda wa Gaza na kufuatia kuidhinishwa sheria nyingine ya kuharamisha uhusiano na utawala wa Kizayuni, alisema.

Pia inaendana na kutimiza wajibu wa kibinadamu, kidini na kimaadili, alisisitiza.

Kutumia neno “Israeli” kunaweza kwa namna fulani kuwa ni aina ya kuhalalisha utawala  Kizayuni ambao unazikoloni ardhi za Palestina, Almuayid alisema.

Agizo kuhusu marufuku hiyo lilitolewa mnamo Desemba 2023 lakini limechapishwa hivi punde kwenye vyombo vya habari.

Mnamo Mei 2022, Bunge la Iraq lilipitisha sheria inayoharamisha nchi hiyo kuanzishaa uhusiano na utawala wa Kizayuni.

Kupitishwa kwake kuliimarisha sera isiyobadilika na ya zamani ya nchi hiyo ya Kiarabu ya kukataa kuutambua utawala unaoukalia kwa mabavu.

 

4194416

Kishikizo: iraq utawala wa israel
captcha