Kwa mujibu wa taarifa, qarii huyo kijana amefariki kufuatia mshtuko wa moyo.
Qarii Mahmoud alikuwa ni mwenyeji wa kijiji cha Shabana katika jimbo la Sharqia la nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Baba yake anasema Mahmoud alihifadhi Qur’ani Tukufu utotoni. Kutokana na sauti yake nzuri alianza kujifunza qiraa ya Qur’ani Tukufu kutoka kwa wasomi bingwa nchini humo.
Mwendazake alikuwa anajishughulisha Zaidi katika qiraa ya Qur’ani na kwafunza Qur’ani watoto na vijana kijini kwake na vijiji vya karibu.
Misri ni nchi ambayo imepata umashuhuri duniani kutokana na idadi kubwa ya wasomaji Qur’ani hasa wale wenye vipaji vya kipekee.