IQNA

Binti wa miaka 14 ashinda mashindano ya Qur’ani Al-Azhar

14:28 - September 30, 2021
Habari ID: 3474364
TEHRAN (IQNA)- Binti Mmisri ameshinda mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Qur’ani ambayo yameandaliwa na Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini humo.

Fatima Atif al Bindary, 14, ameshinda mashindano hayo yaliyokuwa  ambayo yalishirikisha wanafunzi milioni 13 kote Misri.

Fatima ni mwanafunzi wa shule ya sekondari katika mji wa al Kharijah katika jimbo la al Wadi al Jadid.

Baba yake Fatima anasema bintiye alianza kuhifadhi Qur’ani akiwa na umri wa miaka 9. Aidha Fatima amehifadhi hadithi zaidi ya 6000 za Mtume Muhammad SAW.

4001251

captcha