IQNA

Ugaidi

Hisia mseto kufuatia Mauaji ya Ayman al Zawahiri

20:24 - August 02, 2022
Habari ID: 3475567
TEHRAN (IQNA)- Mauaji ya Ayman al Zawahiri, kinara wa mtandao wa kigaidi wa al Qaeda katika operesheni ya droni iliyofanywa na wanajeshi wa Marekani, yamepokewa kwa hisia tofauti ya duru za kisiasa za nchi hiyo.

Mapema leo asubuhi, rais wa Marekani, Joe Biden ametangaza habari ya kuuawa Ayman al Zawahiri katika shambulio la ndege isiyo na rubani lililofanywa na wananchi wa Marekani nchini Afghanistan. Baada ya kutangazwa habari hiyo kumezuka hisia tofauti kutoka kwa wanasiasa wa Marekani akiwemo seneta wa chama cha Republican, Michael McCau ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya uhusiano wa kijeni ya Congress ya Marekani ambaye amesema kuwa, mauaji ya Ayman al Zawahiri yamethibitisha kwamba Biden amewaambia uongo wananchi wa Marekani.

Amesema, mwaka mmoja uliopita, Biden aliongopa alipodai kuwa kundi la al Qaeda haliko tena Afghanistan. Hivi sasa anatangaza kuwa mkuu wa kundi hilo ameuliwa na jeshi la Marekani wakati al Zawahiri ni katika watu wa asili waliopanga mashambulio ya Septemba 11 nchini Marekani na alikuwa bado yuko hai licha ya Biden kudai kuwa al Qaida wamemalizwa nchini Afghanistan.

Seneta huyo amedai kuwa, hatua ya Biden ya kuondoa wanajeshi wa Marekani kiholola na kwa sura ya hatari mno huko Afghanistan imefungua mlango wa kurejea tena kundi la al Qaeda nchini humo na hilo amedai ni uthibitisho wa kufeli kikamilifu siasa za Biden nchini Afghanistan.

Biden amedai mapema leo asubuhi kuwa, aliruhusu kufanyika shambulio makini la kumuua Ayman al Zawahiri na akadai pia kwamba, shambulio hilo halikusababisha madhara kwa yeyote katika watu wa familia yake wala raia yeyote wa kawaida.

4075197

captcha