IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu/ 24

Sifa bora za Mwenyezi Mungu katika Sura An-Nur

9:05 - August 22, 2022
Habari ID: 3475662
TEHRAN (IQNA)- Moja kati ya sifa bora na zenye mvuto za Mwenyezi Mungu SWT zinapatikana katika Sura An-Nur ya Qur'ani Tukufu, na kuna tafsiri kadha wakadha kuhusu aya hizo.

Sura An-Nur ni ya 24 katika Qur'ani Tukufu na ni ya Makii, yaani iliteremshwa katika Mji wa Makka na ina aya  64. Ni Sura ya 103 kuteremshiwa Mtume Muhammad SAW.

Sura hii ilipewa jina la An-Nur kwa sababu neno Nur au nuru limekaririwa mara saba ndani yake na pia ndani yake kuna aya ijulikanayo kama Aya ya An Nur.

Wafasiri wengi wa Qur'ani wameitaja aya hiyo ambayo ni ya 35 kuwa ni yenye kutaja sifa bora zaidi za Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu ni Nuru ya Mbingu na Ardhi. Mfano wa Nuru yake ni kama shubaka lenye kuwekwa ndani yake taa. Taa ile imo katika tungi. Tungi lile ni kama nyota inayo meremeta, inayo washwa kwa mafuta yanayo toka katika mti ulio barikiwa, mzaituni. Si wa mashariki wala magharibi. Yanakaribia mafuta yake kung'aa wenyewe ingawa moto haujayagusa - Nuru juu ya Nuru. Mwenyezi Mungu humwongoa kwenye Nuru yake amtakaye. Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu." Sura An-Nur aya ya 35.

Surah ii pia inazungumza kuhusu kanuni na nidhamu katika  uhusiano wa kijamii na familia. Aya za 2-8 za surah ii zimetajwa kuwa miongoni mwa Ayat al Ahkam yaani aya zenye hukumu za fiqhi.

Wakiashiria aya hizi, baadhi ya wafasiri wa Qur'ani wanasema kumfuata kiongozi anayestahiki na mwenye sifa zilizoanishwa na Uislamu katika kutatua masua ya kijamii ni ishara ya Imani na kumuasi kiongozi kama huyo ni ishara ya unafiki na udhaifu wa Imani. Kati ya nukta zingine ambazo tunaweza kuzipata katika aya hizi ni kukatazwa ubinafsi hasa katika masuala ambayo yanahitaji kuwepo ushirikiano na mashauriano. Aidha aya hizo zinaashiria umuhimu wa kuwa na kiongozi katika jamii na kwamba kumtii kiongozi mstahiki ni ishara ya amani. Aidha tunapata funzo kuwa kuna haja ya kuheshimu na kuzingatia nidhamu katika jamii.

Sura hii pia inajadili uhusiano baina ya wanaume na wanawake na kadhia ya zinaa na adhabu za watendao uovu huo. Halikadhalika katika Sura An-Nur kuna maelezo kuhusu kanuni za Hijabu, ndoa na masharti ya ndoa, na kanuni za kifamilia kati ya maudhui zingine.

Habari zinazohusiana
captcha