IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu / 37

Sura As-Saaffat: Walio katika mstari wa kuwakabili wenye kukanusha Tauhidi

21:20 - October 28, 2022
Habari ID: 3476001
TEHRAN (IQNA) – Kuna makundi mbalimbali ya watu wanaokataa au wanaokana kuwepo kwa Mwenyezi Mungu au upweke wake. Mungu ametuma adhabu kwa baadhi yao na kuwapa baadhi ya wengine fursa ya kutubu huku akieleza ni hatima gani inayowangoja ikiwa hawatafanya hivyo.

Surah As-Saaffat ni sura ya 37 ya Qur'ani Tukufu na yenye aya 182 iko katika Juzuu ya 23 ya Qur'ani Tukufu. Ni Makki na ni Sura ya 58 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Saaffat maana yake ni wale walio kwenye mstari. Inasemekana kuwa inarejelea malaika au waumini ambao wako kwenye mstari wakati wa Sala. Neno Saaffat linakuja katika Aya za kwanza na kwa hiyo jina la Sura.

Dhamira ya jumla ya sura hii ya Qur'ani Tukufu inaelezea Tauhidi (imani ya Mungu mmoja) na kukataa maoni ya makafiri kuhusu Mwenyezi Mungu.

Inatoa sababu za kuthibitisha upweke wa Mwenyezi Mungu, inawaonya wakanushaji na kuwapa habari njema waumini. Inazungumza juu ya nini itakuwa hatima ya vikundi vyote viwili.

Sehemu ya Surah As-Saaffat inahusu hadithi za baadhi ya Mitume wa Mwenyezi Mungu, akiwemo Nuhu (AS), Ibrahim (AS), Ishaq (Isaac), Musa (AS), Harun (AS), Lut (AS), Ilyas ( Eliya) na Yusus (AS).

Aya zinazomhusu Nabii Ibrahim (AS) zinazungumzia maisha yake kwa undani zaidi, ikiwa ni pamoja na kuhusu ujumbe aliopewa Ibrahimu (AS) kumtoa mwanawe kafara, huku Mwenyezi Mungu akiutaja kuwa ni mtihani ulio dhahiri.

Suala jengine lililotajwa katika Sura hii ni Al Yasin. Kuna maoni tofauti kuhusu maana ya Al-i Yasin hapo. Wengine wanasema inawahusu Ahl-ul-Bayt (AS), yaani familia ya Mtukufu Mtume Muhammad (SAW), ambayo ina maana kwamba Mtume (SAW) ameitwa Yaseen. Baadhi ya wengine, ingawa, wanasema inapaswa kusomwa “El-Yasin”, ambayo inamrejelea Mtume Ilyas (AS).

Habari zinazohusiana
captcha