IQNA

Sura za Qur’ani Tukufu /20

Sura Taha; Mafunzo ya Uongozi na Usimamizi

8:22 - October 18, 2022
Habari ID: 3475951
TEHRAN (IQNA) – Moja ya hadithi zilizotajwa katika Sura tofauti za Qur’ani Tukufu ni ile ya Nabii Musa (AS).

Sura Taha ni moja ya sura za Qur’ani Tukufu ambamo kisa cha Musa (AS) kimesimuliwa na mtu anaweza kuona uongozi na mkakati wa usimamizi wa Mtume huyu wa Mwenyezi Mungu, hasa anapokabiliana na Firauni.

Sura ya 20 ya Qur’ani Tukufu ni Sura Taha. Ina aya 135 na iko katika Juzuu ya 16 ya Qur’ani. Ni Sura ya Makki na Sura ya 45 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume (SAW).

Sehemu kubwa ya Sura Taha inarejelea kisa cha Nabii Musa (AS) na kaka yake Harun. Pia inataja kisa cha Hadhrat Adam (AS) na kufukuzwa kwake peponi.

Uumbaji, Ufufuo, imani ya Tawhid, msisitizo juu ya wastani katika kila kitu na kurejea kwa utukufu wa Qur’ani na baadhi ya sifa za Mwenyezi Mungu ni miongoni mwa masuala mengine yaliyotajwa katika Sura hii.

Surah Taha inasimulia kisa cha Nabii Musa (AS) kutoka nyanja tofauti na sura nyingine kwani zaidi inaangazia mikakati yake ya uongozi na usimamizi.

Jambo la kwanza katika uongozi na usimamizi wake ni kutafuta msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu: “Musa) akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Nikunjulie kifua changu, Na unifanyie nyepesi kazi yangu.’” ( Sura Taya aya za 25-26 )

Jambo la pili ni kujaribu kujua udhaifu na nguvu za mtu, jambo ambalo ni muhimu katika usimamizi na uongozi: “Na ulifungue fundo lililo katika ulimi wangu, Wapate kufahamu maneno yangu.” (Sura Taya aya za 27-28)

Hapa Musa (AS) anamwomba Mungu kusaidia kufanya mazungumzo yake yaeleweke kwa kila mtu na yenye matokeo.

Katika uongozi na usimamizi wake, kazi ya timu pia ni muhimu sana. Moses (AS) anamchagua kaka yake Harun kwa kazi ya pamoja kwa vile anafahamu uwezo na umahiri wake.

Habari zinazohusiana
captcha